EACC YASHUTUMIWA KWA KUFUFUA UPYA KESI INAYOHUSU UNUNUZI WA MAHINDI POKOT MAGHARIBI
Wanaharakati katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameshutumu tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC kwa kufungua upya kesi inayohusu ununuzi wa mahindi uliotekelezwa na serikali ya kaunti hii ya pokot magharibi mwaka 2017.
Wakiongozwa na Abraham Kibet wanaharakati hao wamesema kesi hiyo ilifaa kukamilika leo baada ya tume ya EACC kukosa ushahidi wa kutosha ila ikachukua hatua ya kuwakamata watu zaidi waliowahusisha na ununuzi huo wa mahindi na hivyo kuanzisha upya kesi hiyo.
Wanaharakati hao sasa wanadai kesi hiyo imeingizwa siasa huku wakimshutumu mbunge wa Pokot kusini David pkosing kwa kuchochea hali hii .
Maswali yaliibuka kuhusu mchakato wa ununuzi wa magunia 20 ya mahindi yaliyofaa kutumika kama msaada wa chakula kwa wakazi eneo la Kacheliba mwaka 2017 hali ambayo ilivutia tume ya EACC kuanzisha uchunguzi uliopelekea kukamatwa maafisa kadhaa wa serikali ya kaunti.