WATETEZI WA MAZINGIRA KAUNTI YA TRANS NZOIA WALALAMIKIA UJENZI WA SOKO KATIKA MSITU WA SWAM


Baadhi ya viongozi wanaotetea mazingira katika eneo la Swam Endebess kaunti ya Trans Nzoia wamesema kuwa ujenzi wa soko unakusudiwa katika msitu wa Swam huenda ukaathiri vyanzo vya maji katika msitu huo.
Watetezi hao wa mazingira wakiongozwa na Hezborn Wandera na Nelson Mokile wamesema kuwa hatua ya kujenga soko hilo ni njia moja wapo ya kunyakua ardhi.
Hata hivyo wamesema kuwa kamwe hawatakubali hilo kutendeka.
Kadhalika watetezi hao wa mazingira wametaka kusitishwa kwa ujenzi huo hadi pale washikadau wote watakapohusishwa huku wakiitaka serikali kununu ardhi mbadala ya kufanya ujenzi huo.