SEKTA YA BODABODA NCHINI INACHANGIA UKUAJI WA TAIFA
Sekta ya bodaboda humu nchini imetajwa kuwa miongoni mwa zinazochangia zaidi katika ukuaji wa uchumi nchini.
Mwakilishi wa wadi ya Kapomboi katika kaunti ya Trans Nzoia Bernad Mlipuko ambaye alikuwa mwendeshaji pikipiki kabla ya kuchaguliwa kuwa mwakilishi wadi amesema kuwa sekta hiyo huchangia shilingi bilioni 357 kwa mapato kila mwaka.
Akizungumza na wanahabari Mlipuko amesema fedha hizo husaidia kuzikimu familia zao na wengine kubuni nafasi za kazi.