WAFANYIKAZI 70 KAUNTI YA BUNGOMA WAHOJIWA NA EACC KWA MADAI YA UFISADI


Tume ya maadili na kukabili ufisadi eacc imewahoji wafanyikazi 70 wa bunge la kaunti ya bungoma kuhusu ufisadi wa shilingi bilioni 3.2
Aidha tume hiyo imewapa majuma mawili kurejesha fedha hizo la sivyo wakamatwe.
Miongoni mwao 63 ni waakilishi wadi ambao wametakiwa kuelezea kuhusu fedha hizo za marupurupu ya krismasi walizopewa kati ya mwaka 2015 na 2016.
Tume ya eacc imewachunguza viongozi hao ambao inadaiwa kila mmoja alipokea kati ya shilingi alfu 20 na 30 za marupurupu ya krismasi.
imesema kuwa wasiporejesha fedha hizo chini ya majuma mawili basi watakamatwa na kushitakiwa.
Hata hivyo baadhi ya wafanyikazi hao wamesema kuwa ni miaka mingi imepita tangu wakati huo na wala hawakumbuki iwapo walipewa fedha hizo au la.
Wafanyikazi wengine wakiwemo maafisa wa fedha wameagizwa kufika mbele ya eacc ili kutoa mwanga zaidi kuhusu matumizi ya fedha hizo.