VISA VYA UHALIFU VYAPUNGUA KODICH KUFUATIA KUFUNGULIWA CHUO CHA MAFUNZO YA UDEREVA
Hatua ya kufunguliwa shule ya kutoa mafunzo ya udereva katika wadi ya Kodich kaunti hii ya Pokot magharibi imepelekea manufaa makubwa kwa vijana wengi eneo hilo.
Haya ni kulingana na mwakilishi wadi wa eneo hilo Philip Palor ambaye amesema kuwa shule hiyo imepelekea vijana wengi ambao waliasi uhalifu ikiwemo wizi wa mifugo kuanza kujitegemea kwa kupata mafunzo kuhusu udereva, akisema wengi wao sasa wamenunua magari yao.
Aidha Palor amesema kufunguliwa chuo hicho kumesaidia kupunguza visa vya ajali za barabarani katika wadi hiyo kwani sasa vijana wengi hasa wahudumu wa boda boda wamepata mafunzo kuhusu sheria za barabarani.