POKOT MAGHARIBI YATAJWA MIONGONI MWA KAUNTI ZILIZOSAJILI WANAFUNZI WA UMRI MDOGO WALIOFANYA MTIHANI WA KCPE
Kaunti ya Pokot magharibi imekuwa miongoni mwa kaunti tano ambazo ziliwasajili wanafunzi wa KCPE wenye umri wa chini ya miaka kumi na miwili na kuwa na idadi ya watahiniwa mia tisa tisini na tisa.
Akizungumza baada ya takwimu hizo kutolewa, mweka hazina katika ofisi ya chama cha walimu KNUT tawi la Pokot magharibi Daniel Siwakei Lopale, amesema juhudi za kuwasajili wanafunzi hao zimetokana na wakazi kuacha wizi wa mifugo na kukumbatia elimu.
Aidha amesema manifesto ya gavana Lonyangapuo ya kuimarisha masomo kupitia kwa ugavi wa pesa za basari kwa wanafunzi wote wa sekondari imechangia pia pakubwa hatua hiyo.
Kaunti ya Bungoma imekuwa ya kwanza kwa watahiniwa elfu mbili mia tano sitini na watano, ikifuatwa na Kericho, Baringo, Bomet huku Pokot magharibi ikiwa ya tano.