VIONGOZI WA MAKANISA TRANS NZOIA WALALAMIKIA KUPUNGUA MATOLEO KANISANI
Viongozi wa makanisa yaliyobomolewa kwenya kipande cha ardhi kinachomnilikiwa na shirika la reli mjini Kitale kaunti ya Trans nzoia sasa wanasema wanapitia wakati mgumu baada ya kupungua matoleo kanisani.
Wakiongozwa na askofu wa kanisa la United Christian Bible Teaching Henry Shivuka, viongozi hao wamesema kuwa idadi ya waumini katika makanisa hayo imepungua na shughuli zao mbali mbali kusambaratishwa ikiwemo miradi mingi makanisani.
Aidha viongozi hao wamesema kuwa wanaotaabika zaidi ni wajane wanaotumia dawa za kukabili makali ya virusi vya HIV na wakongwe huku wakitoa wito kwa serikali kutafakari kuhusu hatima ya watu wanaokalia ardhi ambazo zinatwaliwa na serikali kabla ya kuchukua hatua yoyote.