SERIKALI YA KAUNTI YA TRANS NZOIA YAANZISHA MPANGO WA KUTOA MATIBABU YA SARATANI YA UZAZI
Serikali ya Kaunti ya Trans-Nzoia Kupitia kwa wizara ya afya imezindua mpango maalum wa kutoa matibabu ya Saratani ya uzazi kwa akina mama walio kwenye umri wa uzazi na kutoa hamasisho ya chanjo ya HPV kwa wasichana wenye umri ya miaka 10 na kurudi chini kwa siku 50 sijazo.
Kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango huo waziri wa afya kaunti ya Trans-Nzoia Clare Wanyama ametoa wito kwa akina mama kujitokeza kwa wingi na kukaguliwa kwani hatua hiyo itasaidia kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na saratani ya uzazi.
Wakati huo huo Bi Wanyama amesema ni asilimia 4% pekee ya wamawake ambao wamechunguzwa dhidi ya saratani hiyo Kaunti ya Trans-Nzoia akisema mpango huo utasaidia kuongeza idadi hiyo maradufu.
Kwa upande wake Mshirikishi wa afya ya uzazi Kaunti ya Trans-Nzoia Bi Selpha Amuko amesema mpango huo wa siku 50 unalenga kupeleka huduma hiyo karibu na mwananchi akisema kwa ushirikiano na PIC 4C wameweza kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya 60 na mashine 10 zimetengwa kwa shughuli hiyo.