WAKAZI WA POKOT MAGHARIBI WAHIMIZWA KUUNGA MKONO MPANGO WA UPATANISHI BBI
Seneta wa kaunti hii ya Pokot Magharibi Samwel Poghisio ameendelea kupigia debe mpango wa upatanishi BBI pamoja na mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020.
Akizungumza katika mahojiano na wanahabari, Poghisio amesema kuwa BBI ina manufaa makubwa kwa wakazi wa kaunti hii huku akitoa wito kwa viongozi kutoka kaunti hii kuungana kuhakikisha kuwa mpango huu unaungwa mkono na kila mmoja.
Aidha Poghisio amesema kwa sasa kampeni za kupigia debe mpango huo zimesitishwa kutokana na janga la corona na kesi zilizopo mahakani, ila wanasubiri ripoti ya kamati ya pamoja ya bunge la taifa na seneti kuhusu mpango huo kabla ya kubaini mwelekeo.
Kando na hayo seneta Poghisio ametoa wito kwa viongozi katika kaunti hii ya Pokot Magharibi kusitisha siasa zisizo na mwelekeo na kushirikiana kuhakikisha amani inadumishwa eneo la tiati ili kuruhusu shughuli muhimu kutekelezwa.