MBUNGE SAMUEL MOROTO AACHILIWA KWA DHAMANA


Mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto amefikishwa katika mahakama kuu ya Kitale ambapo amekana mashataka dhidi yake ya kuwaongoza wenyeji kuharibu mali ya serikali.
Akifikishwa mbele ya hakimu mkuu Makila S.N, Moroto anadaiwa mnamo Aprili tarehe 6 na 7 mwaka wa 2017 aliwaongoza wenyeji waliokuwa na mifugo zaidi ya 100 kuvamia shamba la Suam Ochards ikiwa mali ya shirika la ustawishaji kilimo nchini ADC ng’ombe hao wakiharibu zao la mhindi yenye dhamani ya shilingi milioni 7.9.
Kiongozi wa mashtaka hata hivyo aliwasilisha ombi la kutaka mbunge huyo kunyimwa dhamana kwa msingi kwamba atahitilafiana na ushihidi na mazoea yake ya kukosa kuhudhuria vikao mahakamani.
Moroto aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 500 pesa taslimu au bondi ya shilingi milioni moja
Kesi hiyo inatarjiwa kutajwa Machi 15 upande wa mashtaka nao ukiashiria kumuongezea mashtaka zaidi.