GAVANA LONYANG’APUO AWASHAURI VIJANA KUKUMBATIA VYAMA VYA USHIRIKA ILI KUPATA MIKOPO
Gavana wa kaunti hii ya Pokot Magharibi amewataka vijana kwenye kaunti hii kukumbatia vyama vya ushirika ili kuweza kupata mikopo kwa urahisi na kuanzisha biashara na kuacha mila ya kutegemea mifugo.
Akizungumza katika eneo la Chepareria, gavana Lonyang’apuo amesema kuwa serikali ya kaunti hii itawekeza katika mradi wa chama cha ushirika ili kuwasaidia wenyeji kuimarika kibiashara na hata kupunguza hali ya umaskini.
Hata hivyo wakaazi wameshabikia hatua hiyo wakisema kuwa itawapa fursa ya kuimarisha usalama kwa kuwa visa vya wizi wa mifugo vimekuwa vikiripotiwa kwenye kaunti hii hali ambayo inasababisha utovu wa usalama.