SERIKALI IMESHAURIWA KUWAKAMATA WALIOTEKELEZA MAUAJI YA AFISA WA GSU KAPEDO
Mwakilishi mteule katika wadi ya Mnagei kaunti ya Pokot Magharib Elijah Kasheusheu amelaani na kushutumu utovu wa usalama unaoendelea kushuhudiwa katika eneo la kapedo kaunti ya Turkana.
Kwenye mahojiano ya kipekee na kituo hiki, mwakilishi Kasheusheu amesema serikali inafaa kuwakamata washukiwa waliotekeleza uovu huo mara moja ili sheria ifuate mkondo
Kasheusheu aidha anapinga oparesheni ambayo serikali imeanzisha eneo hilo kuwa huenda raia wasio na hatia wakaumia kufuatia maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi .
Nao wakaazi kaunti ya Pokot Magharibi wakiongozwa na Musa Chepareraka Muyadi ,Paul Kamam na Julias Merikit wamekashifu kitendo hicho na kuilaumu serikali kwa kuanzisha oparesheni mpakani Kapedo badala ya kuwakamata washukiwa kwanza.
Kwa upande wake Stephen Kolimuk kiongozi wa Amani Pokot Magharibi amehoji kuwa ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa inawalinda wananchi wake ikizingatiwa kuwa mwananchi yeyote ana haki ya kuishi popote
Walinda usalama wameanza kushika doria katika eneo la Kapedo baada ya afisa wa GSU kuuliwa hivi majuzi baada ya mkutano wa amani eneo la Kapedo juma moja huku wakitumia ndege na magari ya kivita kushika doria huku wakiwasaka wahalifu ambao wameharibu mali ya watu