WAKAAZI WALALAMA KUHUSIANA NA KUPOROMOKA KWA CHUO CHA KIUFUNDI CHEPARERIA POKOT KUSINI
Wakati habari njema za ujenzi wa chuo cha kiufundi cha Chepareria katika eneo bunge la Pokot Kusini zilipo wafikia wakazi mwaka wa 2013,wengi walikuwa na matumaini mengi .
Hata hivyo, miaka 7 sasa,matumaini yao yamedidimia huku wakisalia kuona jengo likiwa limeporomoka kutokana na ujenzi mbaya na msingi.
Jengo la chuo hicho liliporomoka mwaka wa 2017 ilikuwa kifungua macho kwa wakazi, kuendeleza elimu katika eneo hilo ambalo lilitengwa kwa muda mrefu .
Lakini, hili limesalia kuwa ndoto na wakazi wenye ghadhabu wanahitaji majibu kutoka kwa mbunge wa eneo hilo David Pkosing na wizara ya elimu.
Chuo hicho ambacho kinafadhiliwa na serikali kuu kupitia kwa wizara ya elimu na hazina ya maeneo Bunge [CDF].
Kalya radio imebaini kwamba Jengo hilo ambalo linagharimu shilingi milioni 150 limejengwa kwenye ardhi ya ekari 50 katika eneo la Nasukuta limekwama na hakuna chochote ambacho kinandelea hadi tunavyoenda hewani kwa sasa.
Kalya radio pia imebaini kuwa hakuna chochote ambacho kinaendelea kwenye eneo la jengo ilihali mwana kandarasi tayari amelipwa zaidi ya shilingi milioni 43 kwa mradi hewa kati ya shilingi 48,743,504 na mradi haupo.
Mkazi wa eneo hilo Dennis Kapchok almaarufu Mulmulwas alidai mbunge wa eneo hilo amepuuza suala hilo na hajawahi kulizungumzia suala hilo licha ya yeye kuleta mwanakandarasi na kuonyesha eneo la kujenga chuo hicho.
Kapchok alisema kuwa kucheleweshwa kujenga upya chuo hicho huenda kukaleta hatari ya vijana ambao walikuwa wakitekeleza maovu kama uvamizi na wizi wa mifugo kurejea kwenye maovu hayo.
Alisema kuwa tangu wakati huo,wakazi walimpea mbunge wa eneo hilo nafasi ya kurekebisha shida hiyo lakini hadi sasa hakuna lolote ambalo limefanyika.
Wakazi hao sasa wanataka kuwa ujenzi wa chuo hicho uanze maramoja na kampuni ambayo ilipewa zabuni hiyo kupokonywa lesini na isifanye kazi nyingine kote nchini.
Kapchok alitoa wito kwa idara ya upelelezi [ DCI] na tume ya kupambana na ufisadi nchini [ EACC] kuchukua hatua dhidi ya idara za mafunzo ya kiufundi na hazina ya maeneo bunge [CDF].
Alitoa wito kwa mbunge wa eneo hilo kuwa na uwazi na kuwaajibika pamoja ama wakazi wakusanye sahihi za kumbandua.
Kapchok alisema jengo hilo liliporomoka na ripoti kulihusu haijatolewa.