WAHUDUMU WA AFYA TRANSNZOIA WAAGIZWA KUREJEA KAZINI AU WAFUTWE
Hatima ya wahudumu wa afya wanaogoma katika kaunti ya Transnzoia haijulikani kufuatia barua iliyoandikwa na uongozi wa kaunty hiyo wa kuwataka kusitisha mgomo huo mara moja la sivyo nafasi zao zitangazwe wazi
Kwa mjibu wa barua iliyoandikwa na kutiwa saini na uongozi wa kaunti tarehe ishirini na mbili mwezi huu masharti makali kumi yametolewa moja wapo ya maagizo hayo ni kuwa mkurugenzi wa wizara hiyo ambaye ametakiwa kufuatilia kwa karibu mienendo ya maafisa wanaogoma na kuyanakili majina iliwasimamishwe kazi
Jingine ni kuagiza maafisa wote walio kwenye likizo kurejea kazini huku wale watakaokaidi agizo hilo vilevile kuonywa kufutwa kazi na waliotuma maombi ya kupandishwa vyeo kufutiliwa mbali
Vilevile maafisa wa nyanjani hawajasazwa kwani wameonywa kwamba huenda watashurtishwa kurejea kazini na kuendeleza masomo yao ya taalum yao kwa mwaka mwingine mmoja iwapo wataendelea kushiriki mgomo huo
Ikumbukwe kwamba chama cha madaktari kmpdu kile cha wauguzi knun na chama cha maafisa wa kiliniki kuco vimeshikilia msimamo kwamba hawatarejea kazini hadi wakati ambapo serkali itatekeleza matakwea yao.