GAVANA KACHAPIN ATAKELEZA MABADILIKO KWENYE BARAZA LAKE LA MAWAZIRI.
Na Emmanuel oyasi.
Gavana wa kaunti ya Pokot magharibi Simon Kachapin ametekeleza mabadiliko kadhaa kwenye baraza lake la mawaziri ambapo baadhi ya mawaziri na maafisa wakuu wamehamishiwa wizara mbali mbali.
Katika mabadiliko hayo waziri wa fedha na mipango ya kiuchumi Paul Woyakapel alihamishiwa wizara ya afya, Joshua Ruto akihamishwa kutoka wizara ya barabara na uchukuzi hadi wizara ya fedha na mipango ya kiuchumi.
Cleah Parklea alihamishwa kutoka wizara ya afya hadi wizara ya biashara, mashirika, viwanda na kawi, Joshua siwanyang akitolewa katika wizara michezo utamaduni, vijana na huduma za kijamii hadi ile ya barabara na uchukuzi.
Waziri wa maji, mazingira, raslimali na mabadiliko ya hali ya anga Lucky Litole alihamishiwa wizara, ya michezo utamaduni, vijana na huduma za kijamii, huku William Petot akipewa wizara mpya ya maji, mazingira, raslimali na mabadiliko ya hali ya anga kutoka ile ya biashara, mashirika, viwanda na kawi.
Katika mabadiliko mengine, gavana Kachapin alimkabidhi Daniel Lopale majukumu mapya katika wizara ya biashara, mashirika, viwanda na kawi kutoka ile ya huduma za umma na vitengo vilivyogatuliwa, Lilian Korinyang akiondolewa katika wizara ya mipango maalum na majanga hadi ile ya taasisi za kiufundi.
Musa Losiangole alihamishiwa wizara ya huduma za umma na vitengo vilivyogatuliwa kutoka ile ya biashara, mashirika, viwanda na kawi, David Chepelion akihamishwa kutoka afisi ya gavana hadi wizara ya mipango maalum na majanga.
Aidha Raphael Kalekem sasa atahudumu katika afisi ya gavana baada ya kuhamishwa kutoka idara ya taasisi za kiufundi.