MITIHANI YA KCSE YAANZA HUKU MIKAKATI IKIWEKWA KUHAKIKISHA USALAMA WA WATAHIWA POKOT MAGHARIBI.

Mikakati yote imewekwa kuhakikisha kwamba mitihani ya kitaifa kwa kidato cha nne KCSE ambayo imezanza jumatatu inafanyika na kukamilika vyema katika kaunti ya Pokot magharibi.

Katika kikao na wanahabari kabla ya kuhanza mitihani hiyo, naibu kamishina wa eneo bunge la Kapenguria Wyclife Munanda alisema kwamba mipango ya kuhakikisha usalama imewekwa hasa katika shule ambazo zinapatikana maeneo ambako kumekuwa kukishuhudiwa utovu wa usalama.

Munanda alitumia fursa hiyo kuwaonya wote watakaojaribu kufanikisha wizi wa mitihani hiyo kwamba idara za usalama kwa ushirikiano na maafisa wa elimu wako macho na atakayepatikana atakabiliwa kulingana na sheria.

“Shughuli ya mitahani katika kaunti hii itaendelea salama kwa sababu mikakati ya kutosha imewekwa kuhakikisha changamoto zitakazotokea zinasuluhishwa haraka. Swala la wizi wa mitihani tumewafahamisha maafisa wetu wote kuhakikisha kwamba halitokei.” Alisema Munanda.

Kwa upande wake mkurugenzi wa elimu katika kaunti hiyo Simon Wamae alisema kwamba jumla ya wanafunzi alfu 15,478 wanafanya mtihani huo.

Alitaja mvua inayoshuhudiwa maeneo mengi ya kaunti hiyo kuwa moja ya changamoto ambazo zinakumba usafirishaji wa mitihani japo akiwahakikishia watahiniwa kwamba mikakati imewekwa kuhakikisha mitihani ihiyo inafika katika vituo hitajika kwa wakati.

“Jumla ya watahiniwa katika kaunti hii ni alfu 15,478. Hawa ni wanafunzi wote wa shule za umma na za binafsi. Kwa sasa, tuna changamoto kubwa ya mvua kwa sababu mvua ni nyingi sana na sehemu zetu nyingi haziwezi kufikika. Lakini tumefanya mipango yote kuhakikisha mitihani inafika vituo vyote.” Alisema Wamae.