WAKENYA WAITAKA SERIKALI KUU NA ZILE ZA KAUNTI KUSITISHA SIASA ZA BBI NA KUSHUGHULIKIA WAHUDUMU WA AFYA
Wakenya wa tabaka mbalimbali wanazidi kutoa wito kwa serikali kuu na zile za Kaunti kushghulikia matakwa wa wahudumu wa afya ili waweze kurejea kazini na kusitisha mgomo wao ambao unaingia sikua tatu hii leo.
Wakiongozwa na mmjoa wa kiongozi wa jamii ya Kalenjin na mkulima Stephine Sugut kutoka eneo la Moisbridge Kaunti ya Uasin Gishu amesema hatua ya mgomo wa wahudumu wa afya huenda itawathiri wakenya haswa wakati huu taifa ianapo kabiliwa na ongezeko la maambukizi ya covid 19,akitoa wito kwa Rais Kenyatta na Naibu wake William Ruto kusitisha siasa za mabadiliko ya katiba kupitia kwa mchakato wa BBI na badala yake kushughulikia maswala ya wahudumu wa afya nchini.
Kwa upande wake mmoja wa Mfanyibiashara mjini Moisbridge Bob Rono amesema licha ya changa moto wanayopitia Wakenya kutokana na janga la Covid 19 wakenya wengi wametatizika pakubwa kiuchumi, hivyo mjadala inayofaa kushughulikiwa na serikali kwa sasa ni jinsi ya kukwamua uchumi wa taifa.