WAUGUZI KAUNTI YA BUNGOMA HATIMAYE WASITISHA MGOMO WAO


Wauguzi katika kaunti ya Bungoma ambao wamekuwa kwenye mgomo kwa siku 48 wamesitisha mgomo wao baada ya kuafikiana na serikali ya kaunti hiyo kukusu matakwa yao.
Wauguzi hao wamesitisha mgomo wao mda mfupi tu baada ya chama chao cha kitaifa nchini KNUN kutangaza mgomo mkubwa kote nchini kwanzia siku ya jumatatu wiki ijayo.
Wakizungumza na wanahabari, katibu mkuu wa chama hicho Seth Panyako amesema kuwa hatua hii ni kulalamika hatua ya serikali kupuuza matakwa yao.
Panyako aidha amesema kuwa licha ya wao kulegeza misimamo yao hakuna mkutano wowote ambao umeitishwa na magavana ili kuafikiana.
Mwenyekiti wa chama hicho Joseph Kwasi hata hivyo amesema kuwa kama wahudumu wa afya hawatakubali kuweka maisha yao hatarini.