TRIPPIER ANA NIA YA KUJIUNGA NA BAYERN JANUARI HII.

Callum Wilson na Kieran Trippier

Newcastle United wamekataa ofa ya Bayern Munich kumnunua beki Kieran Trippier, 33.Trippier ana nia ya kujiunga na Bayern Januari hii ikiwa wanaweza kukubaliana na Magpies.Newcastle pia wamekataa ofa ya mkopo kwa mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson kutoka Atletico Madrid lakini wanaweza kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ikiwa ofa ya kudumu itatolewa.