TESTESI KUU ZA SOKA ULAYA


Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amesema kwamba klabu yake inahitaji kumsajili beki mwengine wa ubavu wa kushoto atakayemsaidia beki wa sasa wa nafasi hiyo kieran tierney. Maneja huyo wa the gunners ameyasema hayo baada ya arsenal kuwaachilia mabeki Seed Kolasinac pamoja na Papastathopoulos Sokratis kuondoka. Kuondoka wa wawili hao arteta amesalia na winga bukayo saka na kiungo ainsley maitland niles kama wachezaji mbadala wa kieran tierney.
Jarida la bild ya kule ujerumani imeripoti kwamba mshambuliaji wa leicester city mwenye umri wa miaka 24 kielechi iheanacho, mchana nyavu wa the reds mweneye umri wa miaka 25 divock origi pamoja na mshambuliaji wa nice mwenye umri wa miaka 23 kasper dolberg, wako katika orodha ya washambuliaji wanaosakwa na klabu ya rb leipzig ya kule ujerumani
Leicester city imesitisha mpango wake wa kutaka kumsajili kiungo wa kati wa intermilan na raia wa taifa la denmark mwenye umri wa miak 28, christian eriksen. Kulingana na jarida la telegraph ni kwamba the foxes wamechukuwa hatua hiyo baada ya kiungo huyo wa kitambo wa spurs kudaisha mshahara wa kima cha pauni 300,000 kila wiki.
Mabingwa wa bundesliga na ulaya bayern munich wamethibitisha haja yao ya kutaka kumsajili beki wa kati wa rb leipzig mfaransa mwenye umri wa miaka 22 dayot upamekano. Bayern munich hata hivyo watalazimika kutoa ofa isiyopunguwa pauni milioni 40 ili kufanikisha uhamisho huo. Hayo ni kwa mujibu wa jarida la mirror ya kule uingereza.
Beki huyo pia anaandamwa na klabu za manchester united, manchester city pamoja na chelsea ambao vilevile wanamlenga dayot upamecano na wanasubiria msimu wa uhamisho wa majira ya joto barani ulaya ili kuanzisha mazungumzo ya kusajili beki huyo.
Jarida la sport ya kule uhispania imeripoti kuwa licha ya klabu mbalimbali kuonesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa real madrid na taifa la norway mweye umri wa miaka 22, martin odegaaerd, beki huyo kwa sasa anakaribia kukamilish uhamisho wa kjiunga na arsenal kwa uahmisho wa mkopo. Maneja wa arsenal mikel arteta anasemekana anataka dili hiyo ikamilike amkimtaja kiungo huyo kama atakayesaidia kuchukua nafasi iliyoachwa na mesut ozil aliyejiunga na fenerbahce.