MAAFISA WA NOC-K NA AK WAWATEMBELEA WANARIADHA KAPTAGAT


Maafisa wa kamati ya olimpiki humu nchini NOC-K pamoja na maafisa wa shirikisho la riadha nchini AK-atheletic Kenya wamezuru kambi ya mazoezi ya wanariadha ya Global Sports Communication kule Kaptagat kwenye kaunti ya Elgeyo-Marakwet.
Maafisa hao wamefanya ziara hiyo kwa lengo la kufuatilia maandalizi ya wanariadha watakaowakilisha taifa katika mashindano ya olimpiki duniani inayotarajiwa kuandaliwa mwezi Agosti kule Tokyo Japana baada ya kuahirishwa mwaka uliopita kutokana na janaga la corona.
Wakiongozwa na maneja mkuu wa kikosi cha taifa cha olimpika Barnaba Korir ,maafisa hao walikutana na bingwa na mshikilizi wa rekodi ya olipmiki duniani kwa riadha Eliud Kipchoge, Bingwa wa dunia wa mbio za nyika Geoffrey Kamworor pamoja na bingwa wa mbio za jiji la Chicago na London marathon Brigid Kosgei miongoni mwa wanaridha wengine.
Kando na kuzuru kambi ya maoezi ya Kaptagat maafisa hao pia wamemtemblea mshindi wa olimpiki wa medali ya shaba upande wa urushaji mkuki Julias Yego katika kambi yake ya mazoezi mjini Eldoret ambapo walimpokesa kitita cha shilingi elfu mia tisa ya kufanikisha maoezi yake .