LAMPARD CHINI YA PRESHA KUBWA


Mnoaji wa chelsea muimgereza frank lampard amekiri kwamba anakabiliwa na presha kali pale stamford brige kutokana na misururu ya matokeo duni walioandikissha vijana wake katika mechi zao za hivi majuzi.
Kipigo cha magoli mawili kwa nunge kutoka kwa leicester city siku ya jumanne wiki hii imwzidisha presha kwa lampard hata zaidi .
Licha ya frank lampard kukiri anapitia hali hiyo,amesisitiza kwamba swala la iwapo ataendelea kuwanoa the blues au la haipo miongoni mwa maamuzi anayofaa kufanya .
Mnoaji huyo wa chelsea kwa sasa anapitia wakati mgumu katika taaluma yake ya kufundisha soka ikiwa hadi kwa sasa amepoteza mechi tano kati ya mechi saba za mwisho walizocheza chelsea.
Haya yanajiri huku kukiwa na tetesi za huenda lampard akatimuliwa na aliyekuwa maneja wa kitambo wa kalabu hiyo baina ya mwaka wa 2007- 2008 avram grant kuteuliwa tena.