KALVIN PHILIPS HAENDI MAHALI.

Tetesi za soka.

Manchester City haina mpango wa kumuuza kiungo wake wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips msimu huu wa joto, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kucheza mechi chache tu tangu kuhamia Ettihad kutoka Leeds United.Hata hivyo, Phillips anasemekana kuwa atakua tayari kuondoka City huku kukiwa na hofu kwamba kukosa muda mwingi wa kucheza kunaweza kuathiri nafasi yake ya kuchaguliwa kwenye kikosi cha England.