Aston Villa Yamteua Aliyekuwa Kocha wa Arsenal Unai Emery Baada ya Steven Gerrard Kutimuliwa.
Aston Villa wamemteua kocha wa Villareal, Unai Emery kuwa kocha mpya wa klabu hiyo baada ya Steven Gerrard kupigwa kalamu Emery atawachana na majukumu yake Uhispania, ambapo kwa sasa Villareal inashikilia nafasi ya 7 licha ya kufuzu kwa mchuano wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msumu uliopita Hii itakuwa mara ya pili kwa Emery kufunza klabu ya Ligi Kuu Uingereza baada ya kuongoza Arsenal kutokea 2018 hadi 2019.
Emery anajiunga na klabu hiyo akijivunia matokeo bora yaliyomshuhudia akishinda mataji kadhaa ya Ligi ya Uropa.
Katika taarifa Aston Villa walisema: “Unai anajiunga akitokaa Villarreal, ambayo aliiongoza kwa mafanikio katika Ligi ya Uropa kuifunga Manchester United katika fainali mwaka 2021 na pia nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.”
“Ni kocha mwenye uzoefu wa hali ya juu ambaye ameweza kusimamia zaidi ya michezo 900, Unai pia amewahi kuinoa klabu ya Ligi Kuu Uingereza wakati akiwa na Arsenal, na kuwaongoza Gunners kutinga fainali ya Ligi ya Uropa.”
“Pia amefurahia mafanikio makubwa akiwa Sevilla na Paris Saint Germain. Akiwa Seville, alishinda mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Uropa kati ya 2013 na 2016 kabla ya kutwaa ubingwa wa Ligue 1 nchini Ufaransa na vile vile mataji mawili ya Ufaransa, mataji mawili ya Ligi ya Ufaransa na Trophée des Champions mbili. Unai atachukua nafasi hiyo kuanzia Novemba 1 baada ya taratibu zake za kibali cha kazi kukamilika,” iliongeza taarifa hiyo.