Kocha wa St Anthony Kitale Mayoyo amewaonya wapinzani kutarajia kivumbi mwaka huu

Peter Mayoyo {katika} katika hafla moja ya mashindano moja mwaka uliopita, Picha/Maktaba
Na Emmanuel Oyasi,
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya shule ya upili ya St. Anthony Kitale katika kaunti ya Trans nzoia Peter Mayoyo amewaonya wapinzani kutarajia kivumbi akibainisha kuwa hawawezi kurudia makosa yaliyofanywa wakati wa fainali za kaunti za mwaka jana ambapo walishindwa na St. Joseph Kitale 2-0.
Mayoyo anasema wamejifunza kutokana na makosa yaliyopita na tayari wameanza maandalizi mapema kuelekea michezo ya muhula ujao.
“Hii ni moja kati ya timu bora ambazo nimewahi kuunda katika maisha yangu ya ukocha, tulianza maandalizi mapema mwaka jana, tumecheza mechi za kirafiki za kiwango cha juu sana na ninawahakikishia vijana hawa wana nia ya kushinda, kuna ushindani mzuri kati ya wachezaji na kazi nzuri ya timu; hadi sasa nimefurahishwa sana na ninachokiona,” alisema.
Kocha huyo mkuu aliendelea kuzungumzia michuano ya hadhi ya juu na mechi za kirafiki ambazo wamekuwa wakicheza na kusema wako tayari kukabiliana na wapinzani wowote watakaojitokeza.
Timu hiyo ya St. Anthony Kitale ilishinda taji la kitaifa la kandanda mara ya mwisho mwaka 2023, na wanatumai kuiga ushujaa wa zamani na pia kufuata nyayo za wenzao wa mchezo wa magongo, walifia kiwango cha kitaifa, na ni miongoni mwa timu zinazoshiriki Michezo ya Shule ya Muhula wa 1, inayoendelea jijini Mombasa kwa sasa.